Umoja vituo, klabu za mazoezi waanzishwa Arusha

ARUSHA: KLABU na vituo vya mazoezi jijini Arusha zimeazimia kuanzisha umoja wenye lengo la kuongeza Ushirikiano katika kuhamasisha na kuiongoza jamii katika kufanya Mazoezi.

Katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika ukumbi wa Four Points by Sheraton jijini hapa, kiliwakutanisha wadau mbalimbali wa vituo vya mazoezi na klabu zake (Gym na Jogging Club) ambao walikutana na Ofisi ya Halimashauri ya jiji iliyoongozwa na Ofisa Michezo Benson Maneno.

Kikao hicho kilihitimishwa kwa kuteua uongozi wa muda ambao watasimamia na mara baada ya kukamilisha taratibu zote Uzinduzi rasmi wa chama hicho utafanyika.

Viongozi hao wataongozwa na Mwenyekiti ni Alex Felix,Katibu Athuman Njiku, huku wajumbe kuwa ni pamoja na Leornad Lema, Angel Nyalu na Godfrey Lema.

Akizungumza katika kikao hicho ,Ofisa michezo na Utamaduni wa Halmashauri ya jiji la Arusha Benson Maneno amesema kuanzishwa kwa Chama hicho kutawezesha kuongeza na kuimarisha Umoja kwa vyama na klabu za mazoezi zijulikanazo ‘Gym na Jogging Club ‘.

“Pia vitasaidia kutoa Elimu ya mazoezi na kuwawezesha watu kufanya mazoezi kwa utaratibu kwa kuzingatia usalama wao kwani vyama hivyo vitakuwa na ishirikiano mkubwa na vyombo vya usalama,” amesema Maneno.

Ameeleza kuwa Arusha ni kitovu cha utaliu na mikutano hivyo uanzishwaji wa vyama utatoa fursa mbalimbali kutokana na ubunifu na uendeshaji wake na kusema changamoto za maeneo ya wazi kwa ajili ya mazoezi serikali inaendelea kuzifanyia ufumbuzi lengo ikiwa ni kuhakikisha jamii zinashiriki katika suala la kuimarisha afya zao.

Aidha wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho viongozi hao wameeleza kuwa Kuwepo kwa chama utaongeza Umoja na ushirikiniano katika masuala mazima ya Michezo jijini Arusha.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button