Umoja wa wazazi CCM wajipanga uchaguzi mkuu

UMOJA wa Wazazi Tanzania wa Jumuiya ya Chama cha Mapinduzi (CCM) umesema wanachama wa jumuiya hiyo wako tayari kuingia kwenye uchaguzi wakati wowote licha ya kusikia kuna baadhi ya vyama vya siasa vinataka kugombea uchaguzi mkuu ujao.
Pia jumuiya hiyo imeandaa kongamano kubwa la kimataifa litakaloainisha mafanikio ya Rais Samia Suluhu Hassan tangu alipoingia madarakani mwaka 2021.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Arusha, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa Jumuiya ya CCM Taifa, MCC, Rajabu Maganya amesema kongamano hilo litafanyika Machi 22, 2025 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa AICC, Arusha.
Maganya amesema CCM ina kiu ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 2025 na katika kuonyesha tayari yake wake imeshatoa kauli mbiu yake ya kazi na utu, tunasonga mbele na kutoa wito kwa watanzania kuepuka watu wanaotaka kususia uchaguzi mkuu.
Wakati huo huo, Maganya ametoa onyo kali kwa wanachama ambao wamekuwa wakitumia majina ya viongozi kutaka kugombea nafasi mbalimbali ndani ya CCM kuacha mara moja na kusema hakuna kiongozi anayeweza kufanya kitendo hicho.



