Umri wanaostahili mkopo wasogezwa hadi 45

OFISA Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Robert Kwela amesema kundi la vijana wanaotakiwa kupata mkopo umri wao umeongezwa kuanzia miaka 18 hadi 45 tofauti na zamani ulikuwa umri kuanzia 18 hadi 35.

Kwela amesema hayo leo kwenye kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani cha robo ya  pili ya mwaka  ambapo baadhi ya madiwani walitaka ufafanuzi juu ya utolewaji wa mikopo hiyo ya asilimia 10 kwa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Advertisement

Amesema utaratibu wa maandalizi ya kuanza kutoa mikopo ulianza kufanyika tangu mwezi Oktoba mwaka huu na kinachoendelea kufanyika ni usimamizi wa mifumo ambao utatumika katika kusajiliwa.

“Katika vigezo vilivyowekwa kundi la wanawake halina vigezo isipokuwa awe kwenye kikundi  cha kuweza kufanya biashara  na Watu wenye Ulemavu wawe wawili au mmoja nakujua sababu ya kujirizusha amekosa mwingine wa kujiunga naye,”amesema Kwela.

Kwela amesema suala la usimamizi wa mikopo zitakuwepo kamati ambazo zinasimamia kuanzia ngazi ya vijiji,kata na Wilaya  ambayo itafanya uhakiki  wa vikundi na  fedha za mikopo iliyotolewa.

“Kama Kuna changamoto huko mitaani wananchi hawaelewi wafike kwenye Ofisi za kata kwenye maeneo yao na fomu za vikundi Zina maswali 15 na kigenzo Cha Ushindi zaidi ni maswali hayo kila mmoja kwenye kikundi ajibu kwa ufasaha kwa asilimia 50″amesema Kwela.

Diwani Viti Maalum, Heritha Makaga katika kikao hicho ameomba ufafanuzi namna ya mikopo ya asilimia 10 kwenye vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu maboresho gani yamefanyika.

Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa  Shinyanga,  Fabian Kamoga amesema kuhusu mikopo  ya asilimia 10 serikali imetoa Muongozo ambao unatakiwa uzingatiwe  wa uhalalishaji wa namna ya ufuatiliaji wa mikopo