Umuhimu matumizi teknolojia bunifu wapongezwa CABSAT 2025

DAR ES SALAAM: KATIKA dunia inayoendelea kubadilika kwa kasi kupitia maendeleo ya kidijitali, umuhimu wa kutumia teknolojia bunifu umeendelea kuwa kitovu cha mijadala ya kimataifa.

Hilo lilidhihirika wakati Mtanzania Joshua Moshi, Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Infocus Studio, alipowasilisha mada yenye mvuto katika kongamano la CABSAT 2025, mojawapo ya majukwaa makubwa ya teknolojia ya utangazaji duniani.

Moshi, aliyewakilisha Tanzania katika tukio hilo la kimataifa lililoandaliwa na YoloLiv huko Dubai, aliangazia kwa kina jinsi teknolojia bunifu inavyoweza kutumika kama chombo cha mabadiliko chanya barani Afrika.

Katika mada yake aliyotoa chini ya kaulimbiu “Uboreshaji ni Muhimu”, alieleza safari ya Infocus Studio kutoka kuwa wazo dogo hadi kuwa kampuni inayoongoza katika utayarishaji wa maudhui ya moja kwa moja kwa kutumia vifaa vya kisasa kama Zamunda na YoloBox. Vifaa hivyo vimeleta mapinduzi katika namna ya kurusha matukio mubashara, kwa ufanisi, haraka, na ubora wa hali ya juu.

“Teknolojia inapotumika kwa kulenga mazingira yetu ya Kiafrika, inaweza kuwa suluhisho la changamoto nyingi za kiutendaji,” alisema Moshi.

Amesema Infocus Studio imekuwa sehemu ya mafanikio ya kitaifa kwa kushiriki kurusha moja kwa moja matukio muhimu.

Katika hotuba yake, Moshi hakusita kutoa shukrani kwa serikali ya Tanzania kwa kuweka mazingira rafiki kwa ubunifu wa vijana, akisisitiza kuwa sera sahihi zimekuwa nguzo ya mafanikio ya kampuni kama yake.

Ushiriki wa Moshi katika CABSAT 2025 ni ishara tosha kwamba Tanzania imeanza kujenga nafasi yake katika anga ya ubunifu wa kiteknolojia duniani. Hadithi yake inabeba ujumbe mzito: kuwa na ndoto kubwa, kutumia teknolojia kwa busara, na kuwa na maono thabiti kunaweza kuifikisha Afrika mahali pa juu duniani.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. as soon as the sender sends the package confirmation and certificate of the validity
    of the transactions data to the consolidated contract in the main network,
    anyone person Orbiter finance can order this confirmation to verify the correctness of.

    Take a look at my blog :: Orbiter fi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button