UN yaipongeza Tanzania uhuru wa vyombo vya habari

UN yaipongeza Tanzania uhuru wa vyombo vya habari

UMOJA wa Mataifa umeipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuimarisha uhuru wa vyombo vya habari nchini ,licha ya kukosolewa vikali na baadhi ya Watanzania wanaodai kwamba uhuru huo unatumika kueneza ushoga na usagaji.

Akizungumza leo mjini Zanzibar katika maadhinisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa (UN) nchini Tanzania, Zlatan Milisic amesema uhuru wa vyombo vya habari ni kichocheo cha kuimarisha haki nyingine.

“UN nchini Tanzania inatambua hitaji hili na itaendelea kushirikiana na serikali, washirika, na vyombo vya habari ili kuimarisha upatikanaji wa habari kwa manufaa ya umma,” amesema Zlatan na kuongeza kuwa:

Advertisement

“Tunaipongeza Serikali ya Tanzania kwa hatua inazoendelea kufanya katika kufungua na kuimarisha vyombo vya habari,” amesema Zlatan.

Sherehe za miaka 30 ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani imeadhimishwa kitaifa mjini Zanzibar, huku Bara la Afrika likiadhimisha siku hiyo nchini Zambia.

Kimataifa, siku hii imeadhimishwa jijini New York katika tukio maalum lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *