UN yajipanga kukabiliana karne 21

MAREKANI : BARAZA Kuu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha makubaliano ya kuyaleta pamoja mataifa yanayotofautiana ulimwenguni kwenye kukabiliana na changamoto za karne ya 21.

Changamoto hizo zinaanzia kwenye zile za mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba hadi vita vinavyoendelea na ongezeko la ukosefu wa usawa na umasikini.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha makubaliano ya kuyaleta pamoja mataifa yanayotofautiana ulimwenguni kwenye kukabiliana na changamoto ya karne ya 21 kutoka zile za mabadiliko ya tabianchi na akili mnemba hadi vita vinavyoendelea na ongezeko la ukosefu wa usawa na umasikini.

Makubaliano hayo yenye kurasa 42 kwa jina la “Mkataba kwa ajili ya Mustakabali” yanawataka viongozi wa mataifa 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kuzigeuza ahadi zao kuwa vitendo vikavyobadili maisha ya zaidi ya watu bilioni nane duniani.

Makubaliano hayo yalipitishwa kwenye ufunguzi wa mkutano wa siku mbili juu ya Mustakabali ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Guterres, hapo jana.

SOMA : Guterres aonya mauaji wafanyakazi UN

 

 

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button