UN yakaribisha misaada ya kibinadamu

GENEVA : UMOJA wa Mataifa umetoa wito wa zaidi ya dola bilioni 47 kwa ajili ya misaada muhimu kwa mwaka 2025.
Taarifa imesema kuwa msaada huo utaweza kusaidia mahitaji ya kibinadamu na kuonya huenda kutaongezeka kwa mizozo na majanga ya kimazingira yatakayosababisha mamilioni ya watu kuhitaji msaada.
Mratibu wa masuala ya kiutu na kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, Tom Fletcher ameviambia vyombo vya habari kuwa dunia inateketea na kukiri kuwa kutakuwa na matatizo mengi.
Kwenye uzinduzi wa Tathmini ya Kimataifa ya Hali ya kiutu. Fletcher amesema mizozo mikubwa huko Gaza,Sudan na Ukraine pamoja na mabadiliko ya tabianchi vinachochea zaidi hali hiyo.
SOMA: Baraza UN kupigia kura azimio la kibinadamu Gaza



