MOROCCO: LICHA ya klabu ya Simba kupoteza kwa 0-1 dhidi ya Wydad AC katika Uwanja wa Marrakech nchini Morocco, bao likifungwa na Zakaria Draoui dakika ya 90+5 katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).
Simba imeonesha kiwango walau cha kuridhisha katika mchezo wa usiku wa jana, tofauti na michezo kadhaa nyuma, hata hivyo wao ndio wanashika mkia. Wamekusanya alama 2 tu katika michezo mitatu.
Tofauti ya Simba na Asec Mimosas kinara wa kundi B ni alama 5. Nafasi ya pili yupo Jwaneng Galaxy akiwa amekusanya alama 4 huku Wydad akiwa na alama 3 pekee baada ya kupoteza michezo miwili ya awali.
Desemba 19, 2023 Simba atarudiana na Wydad katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam ikiwa ni ingwe ya pili.
Kundini, kila timu ina nafasi ya kufuzu, ikiwa imesalia michezo mitatu kwa kila timu. Je, Simba anaweza kupenya katika kundi hili?