UNEP yaiunga mkono Tanzania agenda nishati safi

Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme (kulia) akiwa na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bi. Elizabeth Mrema Julai 11, 2024 jijini Nairobi, Kenya.

SHIRIKA la Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) limeiahidi Tanzania kuiunga mkono katika vipaumbele vya mazingira ikiwemo agenda ya nishati safi ya kupikia.

Hayo yamejiri wakati wa mazungumzo kati ya Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Christina Mndeme amekutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Bi. Elizabeth Mrema jijini Nairobi, Kenya.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika kikao cha pembeni baina ya viongozi hao wakati wa Mkutano wa 11 wa Wawakilishi wa Kudumu wa UNEP uliotarajiwa kumalizika Julai 12, 2024.

Advertisement

Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia Dar es Salaam Mei 8, 2024.
Bi. Mndeme ameishukuru UNEP kwa kuisaidia Tanzania katika utekelezaji wa miradi mbalimbali yenye lengo la kuhifadhi mazingira na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Halikadhalika, ameliomba shirika hilo kuendelea kuunga mkono Tanzania hususan katika utekelezaji wa vipaumbele vya nchi katika sekta ya mazingira vikiwemo agenda ya nishati safi ya kupikia, biashara ya kaboni na uchumi wa buluu.
Bi. Mrema ameishukuru Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa michango yake kwenye agenda zilizowasilishwa na kujadiliwa kwa kipindi chote cha mkutano huo.
Kutokana na hatua hiyo Naibu Mkurugenzi huyo amepokea michango hiyo na kuahidi kuichukua kwa ajili ya kuweka kwenye vipaumbele kwenye mpango kazi wa Shirika la UNEP katika kipindi cha mwaka 2024-2025 kwa ajili ya kuifanyia kazi.
Mkutano wa 11 wa Wawakilishi wa Kudumu wa UNEP unafanyika kwa lengo la kupitia programu za shirika hilo UNEP kwa kipindi cha mwaka 2022- 2023 na kupitia mpango kazi na bajeti kwa mwaka 2023 – 2024.
Pia, katika mkutano huo wajumbe wanapitia utekezaji wa kazi za shirika hilo hususan kwenye masuala ya mabadiliko ya tabianchi, bioanuwai na uchafuzi wa mazingira.
Sanjari na hayo, pia wajumbe wa mkutano huo uliofunguliwa Julai 08, 2024 wamepata wasaa wa kufanya maandalizi ya mikutano ijayo ya Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEA – 7).
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango akikagua jiko wakati maonesho katika Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ya Kupikia lililofanyika Machi 9,2024 jijini Dodoma.
Ofisi ya Makamu wa Rais imejikita katika kuhakikisha uhifadhi wa mazingira kupitia vipaumbele kadhaa. Kwanza, ofisi hii inasimamia na kuratibu juhudi za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na kuhimiza matumizi ya nishati mbadala na teknolojia rafiki kwa mazingira.

Pili, inashughulikia udhibiti wa uchafuzi wa mazingira, ikijumuisha udhibiti wa taka, uchafuzi wa hewa, na maji, ili kuboresha afya ya umma na kuhakikisha mazingira safi na salama.

Tatu, ofisi ya makamu wa rais inajitahidi kuhifadhi na kurudisha mifumo ya ikolojia muhimu kama vile misitu, vyanzo vya maji, na ardhi oevu, kwa kuanzisha programu za upandaji miti na uhifadhi wa ardhi.

Nne, imeweka mkazo katika elimu na uhamasishaji wa umma kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira, ili kuhakikisha ushirikishwaji wa wananchi katika juhudi za kimazingira. Hatua hizo zote zina lengo la kuleta maendeleo endelevu kwa nchi, huku ikilinda rasilimali za asili kwa vizazi vijavyo.

 

4o