UNICEF kusaka dola bilioni 9.9 kusaidia watoto

MAREKANI : SHIRIKA  linalohudumia watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limetangaza kampeni ya kusaka dola bilioni 9.9 kwa ajili ya misaada kwa mamilioni ya watoto walioathirika kwa vita na mizozo mingine duniani.

Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, Catherine Russell, amesema kiwango cha watoto wanaoteseka na wenye mahitaji kimefikia hali ambayo haijawahi kutokea kwenye historia ya dunia.

Fedha hizo zitaelekezwa kwa watoto milioni 109 na kusaidia kwenye miundombinu ya kimsingi ya afya, huduma za afya ya akili, maji na elimu, lishe na mapambano dhidi ya udhalilishaji wa kijinsia.

Nchi zmbazo zitahusika na msaada  huu ni  Afghanistan, Sudan, Congo, Palestina na Lebanon. SOMA:UNICEF yalaani shambulio Uganda

Kampeni hii ya UNICEF inatangazwa wakati operesheni za misaada ya kibinaadamu zikikumbwa na uhaba mkubwa wa fedha kote duniani.

 

Habari Zifananazo

Back to top button