UNRWA yapigwa marufuku Israel

ISRAEL : WABUNGE nchini Israel wamepitisha mswada wa sheria wa kupiga marufuku wa shirika la umoja wa mataifa la kuwashughulikia wakimbizi wa kipalestina – UNRWA kuendesha shughuli zake ndani ya Israel kuanzia mwaka 2025.

Hatua hii ya Israel inaweza ikatishia kazi za shirika hilo huko Gaza hasa ukizingatia inategemea vivuko vya mpakani vya Israel kuingia katika ukanda huo.

Agosti , UNRWA ilisema wafanyakazi wake saba wanadaiwa kuhusika katika mashambulizi ya Oktoba 7 na kuamua kuwafuta kazi baada ya kuendelea kufanya uchunguzi.

Advertisement

SOMA: Mashambulizi ya Israel yanateketeza familia Gaza