MAREKANI : TUME ya Kimataifa ya Uchumi wa Maji- GCEW, imesema tatizo la upatikanaji wa maji litaongezeka na kitasababisha nusu ya uzalishaji wa chakula duniani kuwa hatarini 2050.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa hivi karibuni imeonesha takriban watu bilioni 3 wako katika maeneo ambayo hifadhi ya maji inapungua.
Pia imeonesha tatizo la maji litasababisha kushuka kwa asilimia nane ya Pato la Taifa kwa wastani katika nchi zenye kipato cha juu ifikapo mwaka 2050 na hadi asilimia 15 kwa nchi zenye kipato cha chini. Ingawa maji mara nyingi huchukuliwa kama rasilimali asili.
Kufuati tatizo hili wadau wa maji wameelekezwa kuanza kuchukua hatua ili kudhibiti upungufu wa maji unaotegemewa katika uzalishaji wa chakula.