UPANDE wa mashitaka katika kesi ya tuhuma za kusafirisha kilogramu 1001.
17 za dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili mkazi wa Mikocheni, Dar es Salaam, Hussein Hariri na wenzake wawili umedai upelelezi wa kesi hiyo umekamilika.
Wakili wa Serikali Caroline Matemu alidai hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Mery Mrio.
Matemu alidai mahakamani hapo kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi umekamilika na wanasubiri kuwasilisha taarifa Mahakama Kuu na aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine, ili washitakiwa waweze kusomewa maelezo ya ushahidi.
Hakimu Mrio aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 16, mwaka huu na washitakiwa wataendelea kubaki rumande.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Benson Muro (32) mkazi wa mbezi na Ramadhani Almas (46) mkazi wa magomeni mapipa.
Katika kesi hiyo inadaiwa kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo Machi 17 mwaka jana eneo la Mbezi Chini.