Urusi , China wampongeza Lukanshenko

ULAYA : RAIS wa Urusi Vladimir Putin na yule wa China Xi Jinping wamempongeza rais wa Belarus Alexander Lukashenko kwa kupata ushindi wa urais.

Aidha Putin amesema uchaguzi wa jana Jumapili umeonyesha bila shaka kuwa kiongozi huyo anaungwa mkono na watu wa Belarus.

Umoja wa Ulaya na wapinzani walioko uhamishoni au magerezani wamekosoa uchaguzi huo wakisema haukuwa huru na wa haki.

Lukashenko ameshinda muhula wa saba mfululizo madarakani na ameikuwa akiiongoza Belarus kwa mkono wa chuma tangu mwaka 1994. SOMA: BELARUS: Lukashenko kuongoza muhula wa saba

Matokeo ya awali yamempa Lukashenko mwenye umri wa miaka 70 ushindi wa asilimia 86 ya kura. Kiongozi huyo amekuwa akiendesha operesheni kali ya ukandamizaji dhidi ya wapinzani tangu maandamano makubwa kufanyika dhidi yake mnamo mwaka wa 2020

 

 

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button