Ushindi muhimu Stars kufuzu AFCON leo

TIMU ya Taifa ya mpira wa miguu ‘Taifa Stars’ leo inashuka dimbani ugenini huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika(AFCON) dhidi ya Ethiopia.

Mchezo huo wa marudiano wa kundi H utafanyika kwenye uwanja wa Martyrs de la Pentecôte uliopo mji mkuu wa DR Congo, Kinshasa.

Advertisement

SOMA: Taifa Stars katika mtihani kufuzu AFCON leo

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam Septemba 4 Tanzania na Ethiopia zilitoka suluhu.

Katika kundi hilo pia Guinea itakuwa nyumbani kuikaribisha DR Congo.

DR Congo inaongoza kundi ikiwa na pointi 12 baada ya michezo minne ikifuatiwa na Guinea yenye pointi sita, Tanzania ipo nafasi ya tatu ikikusanya pointi nne huku Ethiopia ikiwa na mwisho na pointi yake moja.