MBEYA: Mkazi wa Mbeya, Beth Mayunga ameibuka mshindi wa Sh milioni 20 kupitia kampeni ya ‘Ni Balaa’ inayoendeshwa na kampuni ya huduma ya mawasiliano ya Vodacom.
Licha ya kupata kiasi hicho, Beth ana jukumu la kuchagua shule moja ambayo kampuni hiyo ya mawasiliano itaifanyia ukarabati, ikiwa miongoni mwa mikakati wa kusaidia sekta ya elimu hapa nchini.
SOMA: Vodacom ilivyowakumbuka wagonjwa Iringa
Mkuu wa Vodacom Nyanda za Juu Kusini, Abednego Mhagama alimkabidhi mshindi huyo hundi ya Shilingi milioni 20 jijini Mbeya mnamo Novemba 5, mwaka huu.