Ushirikiano Tanzania, China kuibua fursa za ajira

SERIKALI kwa kushirikiana na Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China wanaofanya shughuli zao nchini, imeingia makubaliano ya kutoa ajira kwa zaidi ya vijana 2,000 wa Kitanzania, ikiwa ni juhudi za kutatua changamoto ya ajira nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Ridhiwani Kikwete, amesema kuwa ushirikiano huo unalenga kuwawezesha vijana kufahamu aina ya ajira zilizopo kupitia kampuni mbalimbali za Kichina zinazofanya kazi nchini Tanzania.

“Kwanza kabisa, kijana anapaswa kufahamu aina ya ajira zilizopo na kuweza kuchangamkia nafasi hizo kupitia makampuni yaliyo tayari kuajiri. Lengo kuu ni kupunguza changamoto ya ajira na kuwawezesha vijana wetu,” amesema Ridhiwani Kikwete.

Aliongeza kuwa Wizara inasisitiza ushiriki wa vijana kwa wingi ili kunufaika na nafasi hizo, ambapo baadhi ya mchakato wa mahojiano (interviews) utafanyika moja kwa moja chuoni, hasa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kampuni za China zinazoshiriki katika mpango huo zinajumuisha sekta za kilimo, uzalishaji wa maji, na nyinginezo, yakiwa na lengo la kutoa nafasi za ajira kwa vijana wa Kitanzania.

“Tunashukuru Serikali ya China pamoja na Balozi wa China kwa ushirikiano huu wa kipekee unaosaidia kutatua changamoto ya ajira kwa vijana wetu,” amesema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania, Juma Sharobaro, amesema zaidi ya kampuni 100 kutoka China zimeshajiandaa kutoa ajira kwa vijana wa Kitanzania, kwa idadi inayokadiriwa kufikia kati ya 1,000 hadi 2,000.

“Ili kijana aajiriwe, anapaswa kutembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuonana na wawakilishi wa kampuni zinazoshiriki, ambapo atapata fursa ya kuzungumza nao na kuelewa aina ya kazi wanazotoa,” amesema Sharobaro.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I am now making an extra $19k or more every month from home by doing a very simple and easy job online from home. sxs I have received exactly $20845 last month from this home job. Join now this job and start making extra cash online by following the instructions on the given website………………….. ­­W­­w­­w­­.­­J­­o­­i­­n­­S­­a­­l­­a­­r­­y.­­­C­­­o­­­m­­­

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button