Ushuru vinywaji vya kuongeza nguvu  kupunguzwa

DODOMA; SERIKALI inakusudia kupunguza kiwango cha ushuru wa bidhaa kwenye vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks) vinavyozalishwa ndani ya nchi kutoka shilingi 561 kwa kila lita hadi shilingi 134.2 kwa kila lita.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Fedha, Dk Mwigulu Nchemba, wakati anawasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka 2025/26 bungeni leo Juni 12, 2025.

“Lengo la hatua hii ni kuweka unafuu kwa wazalishaji wa ndani, kuongeza ushindani na kuchochea uwekezaji nchini. Hatua hii inatarajia kupunguza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi milioni 170,” amesema Waziri Nchemba.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button