Usiyoyajua kuhusu soka la wanawake

DAR ES SALAAM; SOKA la wanawake Tanzania linazidi kukua kiasi cha timu nyingi kuanza kusajili wachezaji wa kulipwa kutoka mataifa mbalimbali kwa ajili ya kuongeza chachu ya ushindani.

Lakini pamoja na kukua kuna changamoto kwenye mikataba kwa baadhi ya klabu zinaende sha timu kimazoea huku ny ingine kukiwa na maslahi duni kwa wachezaji kuonesha namna gani zinawanyonya.

Spotoleo liliwatafuta wadau wa soka la wanawake kwa nyakati tofauti kwa ajili ya kuzungumzia kuhusu mikataba ya wanasoka wanawake kuathiri ustawi wao.

Wadau, makocha, viongozi na wachezaji walifunguka akiwemo kwa moja kwa sababu hakuna ushahidi. aliyekuwa Kocha wa JKT Queens, Ally Ally amesema wachezaji wengi wamekuwa wakisaini mikataba yenye maslahi mado go sana. Amesema ukizitoa timu za Simba Queens, Yanga Prin cess, JKT Queens na Mashujaa wengine wanataabika, wa nacheza katika hali kama ya kujitolea, hawana mikataba inayoeleweka.

“Mikataba isiyoeleweka in awafanya kunyonywa maslahi yao wanacheza ligi kuu lakini wengi mishahara yao haizidi sh 200,000 hadi 300,000. mikataba iiyoeleweka ni sawa na ukatili, rahisi kupata ushawishi ikizin gatiwa kuwa wale ni watoto wa kike. Wakilipwa maslahi mazuri in au mapungufu yanapokuja.

Kingine tunajikuta sisi wenyewe tunakubali kujishusha kwa ajili ya kupata timu. awasaidia hata kutoingia katika mtego wa ukatili wa kijinsia kwa sababu kipato wanachokipata kinaweza kusaidia kuendesha familia zao,” amesema mdau huyo wa soka la wanawake.

Ameshauri kuwaTFF wahakik ishe wachezaji wanakuwa na mikataba inayoeleweka wafuatil ie kwa kina, timu inayoshindwa kulipa vizuri basi kuwekwe kanuni za kuwabana. Mwenyekiti wa Soka la Wanawake Tanzania (TWFA), So moe Ng’itu amesema mkataba unakuwa ni baina ya mcheza ji na mwajiri uwe mzuri au mbovu unatokana na mchezaji mwenyewe aliyesaini.

“Inapotokea umekubali kudan ganyika au kurubunika ukasaini mwenyewe ndio yale matatizo Unaweza kuwa unatamani kupata mkataba wa sh milioni moja lakini wewe mwenyewe ukakubali kusaini wa sh 600,000 ukiamini ukisimama kwenye milioni moja wao wenyewe wakakataa au ukakosa timu,”. Somoe amesema klabu zisi wakandamize na kuwashusha, ziangalie mikataba wanayoingia na wachezaji kwasababu ni kesho yao.

Kesi zipo kwa maana wachezaji wenyewe kutoitumikia mikataba yao na klabu kuvunja mikataba isivyo halali. Amesema wachezaji wanapo fuatwa na timu jambo la kwanza hawaangilii vipengelee zaidi ya kuona fedha na kusaini mwisho wa siku wanaondoka kwa kuona kiasi kidogo cha fedha na kuin gia kwenye matatizo na klabu.

“Hii inatokana na baadhi yao kutokuwa na uelewa na mkata ba, hakuna mikataba ambayo inamfanya mchezaji kupoteza taswira yake ya uwanamke,” amesema.

Edna Lema ambaye ni Kocha wa Yanga Princess anasema mchezaji au kocha anapopewa mkataba asipoweza kuuelewa unaweza kumuathiri kwasa babu mara nyingi wachezaji wanakimbilia kusaini bila kuso ma vipengele vya mkataba.

Amesema matokeo yake matatizo yakitokea mcheza ji haudhurii kambini wala mazoezini huenda kinyume na makubaliano ya mkataba. Lakini pia, kukosa elimu ya mkataba na kushindwa kwenda sehemu husika kupata haki zake.

“Mtu amesaini bila kusoma vizuri au bila kupata mtu wa kumfafanulia, wakati mwingine mkataba unaweza kukuongoza, shida kubwa sio kwa wacheza ji bali ni watu wanaojitokeza wanajiita ni mameneja wanaku wa tatizo,”amesema.

Ameeleza kuwa suala la haki kwenye soka la wanawake hawawezi kupata haki sawa na wanaume kwasababu ndio kwanza mpira wa wanawake unaanza kukua.

Mshambulia wa Al Nasr ya Saudi Arabia na Twiga Stars, Clara Luvanga

Kuhusu ukatili wa kijinsia, amesema lipo kila mahali na kwenye soka inawezekana lakini hawezi kuweza wazi moja “Unyanyasaji, rushwa ya ngono vipo inategemea na muhusika aliyekutana na changamoto hiyo, anatakiwa kujitambua na usikubali kupoteza kipaji chako kitumike vibaya,” amesema Ko cha huyo wa Yanga Princess.

Beki na nahodha wa Simba Queens Voileth Nicholas ame sema mikataba mara nyingi ipo vizuri na haiathiri ustawi wao wa kijinsia kabla ya kusaini anataki wa kuwa makini kwa kuipitia na kufanya maamuzi.

“Kwangu sijawahi kukutana na changamoto hiyo ya mkataba, la kini nasikiaga hata nchi za jirani juu ya hilo lakini, tafiti zangu ni lazima mmoja kati ya mchezaji au uongozi anakuwa hajafuata wanayoingia.

Matatizo ya kijinsia siwezi kusema hakuna inaweza kutokea na tunasikia juu juu lak ini wahusika hawakutaka kuwe ka wazi,” amesema Mwenyekiti huyo. mkataba unavyosema,” amese ma beki huyo.Meneja wa Simba Queens Selemani Makanya amesema mikataba inalindwa pande zote mbili, klabu wan apovunja mkataba mchezaji anapewa haki zake.

Amesema kuna baadhi ya kla bu hazifuati taratibu za mkataba kwa wachezaji ikiwemo kutope wa haki zao ikiwemo mishahara na fedha za usajili. “Zamani kanuni ya mkataba inasema mchezaji asipolipwa fedha za usajili au mshahara kwa miezi mitatu mkataba unavunjwa lakini miaka ya hivi karibuni ni miezi miwili. Wachezaji wengi wa kike hawa jui elimu ya mikataba wanay oingia na klabu na inapofika hatu wananyimwa stahiki zao na kukata tamaa ya kuonyesha kip awa chake,” amesema Selemani.

Ameeleza kuwa kutofahamu elimu ya mikataba inapele kea wachezaji wengi kuogopa kwenda kutafuta haki zao katika mamlaka iliyowekwa kama Cha ma cha wachezaji wa zamani na sasa na kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji iliyoundwa na TFF.

Mwenyekiti wa Kamati ya She ria na hadhi za wachezaji Said Soud ameweka wazi kwamba wanapokea malalamiko mach ache kutoka kwa wachezaji wa kike.

“Hayo machache ni kutokana na kiwango kidogo cha fedha, hii inatokana na klabu kunu faika au wachezaji hao kutojua haki zao na elimu ya mikataba Ameeleza kuwa katika kute tea haki na kulinda ustawi wa wachezaji wa kike wapo na mpango wa kutoa semina kwa viongozi pamoja na wachezaji hao kupewa elimu ya mikataba wanayoingia.

“Kwa kuwa tuko kwenye mpango huo, tumeanza kuzu ngumza na bodi ya ligi na TFF wanaoendesha ligi hii kukaa na viongozi wa klabu na wachezaji kuwapa elimu na wachezaji kusimama imara katika ku tambua ustawi wao kwenye makubaliano,” amesema.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button