‘Utawala wa kodi ni kiungo muhimu huduma za umma’

DAR ES SALAAM; Gavana Mstaafu wa Benki kuu ya Tanzania (BoT) Profesa Florens Luoga, amesema utawala wa kodi ni kiungo muhimu kati ya serikali na wananchi katika kukusanya rasilimali za maendeleo na kutoa huduma za umma.

Almesema hayo wakati wa uzinduzi wa kitabu Cha Utawala wa Kodi Tanzania (Administration of Income Tax in Tanzania) kllichozinduliwa Ukumbi wa huduma za Maktaba za Taifa Oktoba 16, 2026 jijini Dar es Salaam.

Profesa Luoga alisema vitabu vinatoa fursa ya kufuatilia mtiririko mzima wa mawazo na kuelewa ikiwa mifumo ya kodi ni ya haki , inaleta ubaguzi na mzigo mzito kwa baadhi ya wananchi.

Luoga alisisitiza umuhimu wa kusoma vitabu vilivyochapishwa badala ya kutegemea usomaji wa juu juu wa mtandaoni.

Naye, mwandishi wa kitabu Dk Njoroge Kimani, ambaye ni wakili wa Mahakama kuu nchini Kenya alisema kuwa kitabu hicho kinalenga kuziba pengo kubwa la maarifa ya kodi linalowakabili walipa kodi pamoja na wataalamu wa sekta hiyo.

“ Mfumo wa sheria za kodi unahitaji tafsiri sahihi, kwani kosa dogo au tafsiri isiyo sahihi ya kifungu cha sheria inaweza kumwingiza mlipa kodi katika hasara kubwa au kujishtaki mwenyewe,”alisema Dk Kimani.

Akitolea ufafanuzi juu ya kitabu hicho Dk Kimani alisema: “Kitabu hiki kinazingatia zaidi taratibu za kila siku za utawala wa kodi kama vile usajili, uwasilishaji wa marejesho (returns), tathmini, pingamizi, rufaa, faini, na marejesho ya fedha (refunds),ambapo ndipo ukiukaji wa kodi unapoamuliwa”.

Kwa mujibu wa Kimani , kitabu hicho kimeandaliwa kwa kuzingatia mahitaji ya wafanyabiashara, walipa kodi binafsi, wahasibu, wakaguzi, washauri wa kodi, mawakili, wanafunzi na wahadhiri wa sheria, uhasibu na fedha.

Amesisitiza kuwa migogoro ya kodi hugharimu fedha nyingi, muda, na kuharibu mahusiano ya kibiashara, hivyo elimu na uwazi katika taratibu hizo husaidia kuzuia migogoro kabla haijatokea.

Aliongeza kuwa kutokana na ushirikiano wa karibu wa kibiashara, kihistoria, na kilugha kati ya Kenya na Tanzania ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, hivyo wawekezaji na wataalamu wengi wanaovuka mipaka wamekuwa wakihitaji uelewa wa wazi kuhusu jinsi mifumo ya kodi inavyosimamiwa kwa vitendo katika nchi wanazofanyia kazi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Uchapaji ya Mkuki na Nyota, Mkuki Bgoya alisema kuwa kuchapishwa kwa kazi hiyo kunaendana na dhamira ya kampuni ya kukuza maarifa ya Kiafrika na kuyafikisha kwa wasomaji ndani na nje ya Afrika.

“ Kampuni hii imewahi kuchapisha kazi za waandishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika pamoja na sehemu nyingine duniani, ikisisitiza kuwa maarifa ya Afrika hayapaswi kubaki ndani ya mipaka ya kitaifa,”alisema Bgoya.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. ❤️ Wasichana warembo na wenye hamu ya kimapenzi kutoka kote duniani wanakungoja; jiunge hapa ……………………………………………………………………………….……> https://da.gd/girls66

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button