KENYA: Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza baraza la jipya la mawaziri kumi na moja kati ya 22 katika baraza lake la mawaziri.
Katika hotuba yake kwa taifa ambayo ameitoa leo Ikulu ya Nairobi, Rais Ruto amesema kwamba idadi ya mawaziri waliosalia itatangazwa wiki ijayo baada ya kikao cha mashauriano.
Rais amesema kwamba uteuzi huo ambao ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali – unafuatia mashauriano katika sekta ya kisiasa katika jaribio la kurudisha amani na utulivu nchini humo.
SOMA: Rais Ruto avunja baraza la mawaziri Kenya
Orodha hiyo pia ilikuwa na Mawaziri sita waliofukuzwa kazi, ambao sasa wanarejea katika wizara tofauti, huku Prof. Kithure Kindiki, Alice Wahome na Adan Duale wakiendelea kushikilia nafasi zao za zamani.
State House, Nairobi. https://t.co/EfY0waXEm3
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) July 11, 2024