Utezi wagombea CCM  ngazi ya mikoa waiva

HATMA ya wanaowania nafasi za uongozi ngazi ya Mkoa katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) itajulikana kesho Septemba 28, 2022.

Taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi  wa CCM, Shaka Hamdu Shaka imesema Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), inaanza vikao vyake vya kawaida kesho  Chamwino mjini Dodoma.

Imesema kuwa pamoja na mambo mengine, vikao hivyo vitakuwa na kazi ya kupokea mapendekezo, kujadili, kupitisha na kufanya uteuzi wa mwisho wa wanachama walioomba uongozi katika ngazi ya mikoa na taifa kwa upande wa jumuiya pamoja na chama.

Amesema vikao hivyo vimetanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika   Oktoba 24 na 25  2022 jijini Dodoma.

Habari Zifananazo

Back to top button