UVCCM endeleeni kuhamaisisha vijana

ZANZIBAR : MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) na UVCCM waendelee kuongeza kasi ya uhamasishaji uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kuhakikisha vijana wengi wanajiandikisha litakapoanza kwa upande wa Unguja hivi karibuni.
Ametoa wito kwa vijana kutobaki nyuma siku ya kupiga kura ili CCM ipate ushindi wa kihistoria na kuendelea kushika Dola.
Dk.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Bweni la Vijana wa Kiume wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM).
“lazima Chama cah mapinduzi kiache alama ya uongozi itakayokumbukwa kwa muda mrefu kwa kufanya mambo makubwa ya maendeleo na miradi ya Chama katika ngazi zote.” Alisema Dk. Mwinyi.
Halikadhalika Dkt.Mwinyi amefahamisha kuwa alama iliyoachwa na Serikali katika Sekta zote za Maendeleo ni lazima pia iachwe ndani ya CCM.
Vilevile Dk.Mwinyi ameipongeza UVCCM kwa kufanikiwa kujenga Jengo hilo litakalotumika kwa harakati mbalimbali za Jumuiya hiyo.

Kwa upande mwingine Dk.Mwinyi amesema Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuunga Mkono juhudi za Jumuiya hiyo kwa hali na Mali ili dhamira ya kuwajenga vijana kuwa wazalendo na kuwapatia mafunzo mbalimbali ifanikiwe.
SOMA: Dk. Mwinyi: Hakikisheni CCM inashika dola
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Taifa,Mohammed Ali Kawaida amesema Kauli ya Mitano Tenani kwa ajili ya viongozi wawili tu ndani ya CCM ambao ni Mwenyekiti wa CCM Taifa,Ndugu Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Mwenyekiti CCM Zanzibar, Ndugu Hussein Ali Mwinyi.




