MWENYEKITI Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Kagera Faris Buruhan amewataka wananchi wa Wilaya ya Ngara mkoani kagera kutowachagua viongozi waongo wasioweza kuleta maendeleo katika jamii.
Faris ameyasema hayo wakati akizungumza na jumuiya ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Omulusagamba iliyopo katika kata ya Omurusagamba wilayani Ngara.
Amewaambia wanafunzi hao dhamira ya kufika katika shule hiyo ni kampeni maalum ya kutafuta kura za Rais Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi.
“Ilani ambayo inatekelezeka ni Ilani ya Chama Cha Mapinduzi ,Ilani ambayo imekuwa mkombozi wa miradi mingi ya maendeleo na hasa elimu, wanasiasa wa vyama vingine wako majukwaani lakini hatujui wanazungumzia nini hawana ilani wanazungumzia kile ambacho akijaandikwa hivyo hakikisha mnawachagua viongozi wa kweli watakao wavusha,” amesema Faris.
Akizungumza na wanafunzi hao ambao wametimiza 10 na 18 kufanya mchakato wa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ili waweze kupata haki ya kupiga kura na kumupigia kura Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwachagua wabunge na madiwani watakaoletwa na Chama Cha Mapinduzi.
Hata hivyo baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya omurusagamba wamesema kuwa wao wapo tayari kujiandikisha katika daftari la mpiga kura ili waweze kumpigia kura Rais Samia ambaye amefanya mambo makubwa katika nchi hii hasa kuboresha miondombini ya elimu,mabweni pamoja na huduma nyingine za maendeleo. katika maeneo yao.
Can you imagine making $18,000 a month while working from home just a few hours a day? I’m doing it, and I never thought it was possible until I found this online opportunity. The work is super easy, and you don’t need any prior experience—just a desire to succeed! I can’t believe how much my life has changed in such a short time. If you’re ready to take control of your income, visit the website and get started today!
Visit This…… http://www.worksprofit7.com/