Uzalendo utawale mawazo, matendo ya vijana

DAR ES SALAAM: UZALENDO ni nguzo muhimu katika ujenzi wa taifa lolote; ni nguvu ya ndani inayomfanya mtu kuthamini nchi yake, kuitumikia kwa moyo mmoja na kuipa kipaumbele katika maamuzi ya kila siku.

Leo, zaidi ya wakati mwingine wowote, tunahitaji uzalendo uongoze mawazo na matendo yetu kutokana na kasi ya mabadiliko ya dunia inavyokwenda.

Kila mmoja wetu ana nafasi ya kipekee katika kuijenga nchi na ili kujenga nchi, kila mmoja anapaswa kuwa mzalendo. Neno hilo haliishii kwenye kupigania mipaka kama ilivyokuwa zamani bali unajidhihirisha katika mambo madogo tunayofanya kila siku.

Tunapolinda mali za umma, kuheshimu sheria, kutenda haki, kufanya kazi kwa bidii na kuchangia katika ustawi wa jamii, tunakuwa tumedhihirisha uzalendo kwa vitendo. Pia, kuhimiza amani, kupinga rushwa na kulinda rasilimali za taifa ni sehemu muhimu ya kuonesha upendo kwa nchi yetu.

Ni lazima tukubali kuwa taifa haliendelezwi na viongozi pekee bali linajengwa na raia kwa kiasi kikubwa hususani wanaoweka maslahi ya nchi mbele ya maslahi binafsi, bila kujali utofauti uliopo wa kidini, kiitikadi, jinsia wala kiumri.

Tunapokuwa na mawazo ya kizalendo, tunafanya maamuzi yanayolenga manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo na tunatumia talanta, elimu na maarifa yetu kuleta suluhisho badala ya malalamiko, tunatumia sauti zetu kuhimiza maendeleo na si kugawa jamii.

Rais Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia taifa, kupitia mazungumzo yake na Wazee wa Dar es Salaam mnamo Desemba 2, 2025 aliwataka wazee nchini kuendelea kuhamasisha amani kwa kuwapatia vijana elimu ya uzalendo na kuwahimiza kuipenda na kuilinda nchi yao.

Hii inatoa msisitizo kuwa vijana wana uwezo wa ama kulijenga au kulibomoa taifa kwa sababu wao ndio kizazi cha leo; kila kitu kipo mikononi mwao, hivyo uzalendo wa vijana utalijenga na kulilinda taifa kupitia mawazo na matendo yao.

Katika kizazi hiki kilichotawaliwa na maendeleo makubwa ya teknolojia na utandawazi, vijana wanapaswa kuongoza mapinduzi ya uzalendo wa kisasa; uzalendo unaoheshimu utofauti, unaokuza ubunifu na unaochochea maendeleo ya kiuchumi.

Taifa lenye watu wazalendo ni taifa lisiloweza kutikisika kwa urahisi; lenye mshikamano na lenye dira ya pamoja, hivyo uzalendo ukitawala mawazo na matendo, tunaweza kuijenga Tanzania yenye nguvu, umoja na mafanikio ya kudumu.

Wazo hili limeandaliwa na Ramla Hamidu, Mwandishi wa Gazeti la HabariLeo

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Single Mom Reveals How She Earns $89k/Yr Working 10 Hrs/Week From Home. Tired of paycheck-to-paycheck living? Meet Kelly from New York—a regular mom who cracked the code to recession-proof income without selling a thing! Now,Big thanks …
    .
    Here is I started____________________ http://Www.Cash43.Com

  2. Google is now paying $300 to $500 per hour for doing work online work from home. Last paycheck of me said that $20537 from this easy and simple job. Its amazing and earns are awesome. No boss, full time freedom and earnings are in front of you. This job is just awesome. Every person can makes income online with google easily……….
    .
    M­­­­­­o­­­­­­r­­­­­­e­ D­­­­­­e­­­­­­t­­­­­­a­­­­­­i­­­­­­l­­­­­­s For Us→→→→→→→→→→ https://Www.Payathome9.Com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button