Uzalishaji taka plastiki wasumbua dunia

KOREA KUSINI : MAZUNGUMZO ya wiki nzima kuhusu mkataba wa kihistoria wa Umoja wa Mataifa kuhusiana na taka za plastiki yamekwisha bila ya wajumbe kufikia muafaka kuhusu taka za plastiki huko mjini  Busan.

Hatua hii ni pigo kubwa katika kukabiliana na uchafuzi unaongezeka wa mazingira  utokanao na taka za plastiki.

Katika mazungumzo hayo,mataifa  zaidi ya 100 yamekubali kuweka kiwango cha uzalishaji wa taka za plastiki ikiwemo Mexico, Panama, Rwanda na Umoja wa Ulaya.

Lakini mataifa yanayochimba mafuta kama Saudi Arabia na Urusi yamepinga vikali hatua hiyo na badala yake yakataka makubaliano hayo yajikite katika njia bora za kutupa taka za plastiki.

Duru hii ya tano ilichukuliwa kuwa ya mwisho ya mazungumzo hayo, lakini sasa mjadala huo utaendelea mwakani. SOMA:  Mikindani wahimizwa kutunza fukwe

Habari Zifananazo

Back to top button