Mikindani wahimizwa kutunza fukwe
JAMII katika Halmashauari ya Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara imetakiwa kuhifadhi maeneo ya rasilimali za bahari (Fukwe) ili kuweka mazalia ya samaki katika hali ya usalama zaidi.
Akizungumza katika halmashauri hiyo mkoani humo wakati wa zoezi la ufanyaji usafi kwenye baadhi ya fukwe zilizopo kwenye manispa hiyo , diwani wa kata ya Shangani katika manispaa hiyo, Abuu Mohamed amesema ameguswa kushiriki usafi huo kwa sababu ni maeneo ambayo yamesahaulika.
Zoezi hilo limeandaliwa na taasisi isiyo ya kiserikali inayojishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii kwenye manispaa hiyo ikiwemo uwezeshaji wanawake, vijana na masuala ya mazingira ya Fb-Empowerment, uliyofanyika kwenye baadhi ya fukwe kama vile makonde beach, jeshini na zingine.
Amesema maeneo hayo watu hupenda kwenda kujipumzisha hasa siku za mapumziko (Weekend) pamoja na siku za kawaida ambapo katika mapumpuziko hayo kunakuwa na chupa za plastiki na uchafu uchafu mwingine unaofanana na plastiki ambao unaenda baharini kuharibu mazalia ya viumbe hivyo.
SOMA: ‘Wekezeni michezo ya ufukweni’ – …
‘’Nimeona ni jambao la msingi sana kwenda kusafisha kule kwasababu ya itaweka mazingira ya fukwe zetu katika mazingira ya usafi na kuweka mazalia ya samaki yakiwa salama zaidi,”amesema Mohamed
Aidha ametoa rai kwa taasisi mbalimbali kwenye manispaa hiyo kuwa ziinge mfano huo ili wote kwa pamoja waweze kuhifadhi fukwe zilizopo katika kata hiyo na maeneo mengine na kusisitiza kwamba, zoezi hilo lisiishie hapo tu bali liwe endelevu.
Meneja wa taasisi hiyo Shakila Hamis amesema moja ya majukumu yao ikiwemo upande wa mazingira wamekuwa ni mawakala wa muda mrefu kwenye utoaji elimu kwa wanawake, vijana na watoto juu ya udhibiti wa taka ngumu aina ya plastiki ambazo huleta athari hasi kwa mazingira ya viumbe hai waishio baharini.
Amesema taasisi hiyo imekuwa na utaratibu wa kuandaa shughuli mbalimbali za kijamii kila baada ya miezi mitatu au minne kwa kushirikiana na vikundi mbalimbali vya usafi kwenye manispaa hiyo ikiwemo Mtwara kuchele na vingine.
SOMA: Gwajima avalia njuga ubakaji ufukweni
Lengo likiwa ni pamoja na kuhamasisha makundi ya vijana na wanawake kwa kushirikiana na serikali kuona namna wanavyoweza kudhibiti uchafu huo usifike baharini.
‘’Katika kuelekea siku ya usafi duniani Septemba 20, 2024, wadau mbalimbali wamehamasishwa kuanza kufanya shughuli za usafi hususani maeneo ya fukwe za bahari ili kudhibiti uchafu wa plastiki kuingia baharini”
“Lakini pia kuhamasisha bahari kuwa safi, tuliandaa zoezi hili kwa kushirikisha ofisi ya manispaa na walipokea kwa mikono miwili na tukaungana nao’’ amesema Hamis