Uzinduzi jezi Kilimanjaro wazo la Kajula

WAZO la uzinduzi wa jezi mpya zitakazotumika msimu wa 2023/2024 kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro lililetwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Iman Kajula. Meneja wa Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Ahmed Ally ameeleza.

“CEO Imani Kajula ndiye mwanzilishi wa wazo la kuzindulia jezi juu ya kilele cha Mlima Kilimanjaro”. Amesema Ahmed Ally.

Baadhi ya viongozi wa klabu hiyo wamewasili Kilimanjaro ambako wataanza zoezi la kuupanda mlima huko katika zoezi la uzinduzi wa jezi Ijumaa hii.

Habari Zifananazo

Back to top button