‘Uzinduzi WCX kuimarisha uchumi kidijitali’

Dar es Salaam; KUZINDULIWA kwa Jukwaa la Wingu Cloud Exchange (WCX) kumeelezwa kutaimarisha kwa kiasi kikubwa uchumi wa kidijitali.

Hatua hiyo imekuja baada ya Kampuni ya Wingu Africa leo Novemba 19, 2025 kuzindua rasmi huduma mpya za Data Center kupitia WCX kupitia mfumo wa kisasa uitwao Private Cloud unaohifadhiwa nchini kwa ajili ya nchi za Afrika Mashariki.

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Wingu Africa, Huneid Ali, amesema WCX imeundwa kutoa mbadala salama na nafuu kwa huduma za cloud za nje ya nchi, huku ikihakikisha usalama na ufanisi wa data za taasisi na biashara.

“Faida za WCX ni pamoja na usalama wa hali ya juu, ufuatishaji wa matakwa ya kisheria, gharama nafuu, na urahisi wa matumizi ukilinganishwa na huduma za kimataifa.

“Kupitia bei za ndani, uwezo wa kusaidia mifumo haraka, na kupanuka papo hapo, jukwaa hili linaziwezesha biashara kukuza matumizi ya teknolojia bila gharama zisizotabirika,” amesema Ali.

Kwa upande wake, Meneja wa Data Center wa Wingu Africa, Bilali Tofika, amesema jukwaa hilo limezinduliwa kwa mara ya kwanza Tanzania na litafika katika masoko mengine ya kampuni hiyo ikiwemo Ethiopia na Djibouti.

Naye Erkan Satik, Mkurugenzi wa Cloud Ecosystem & Alliances wa Wingu Africa, alisema uzinduzi wa WCX ni hatua muhimu katika safari ya kukuza ukomavu wa kidijitali Afrika Mashariki.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button