Venancio Mondlane arejea Msumbiji

MSUMBIJI : KIONGOZI wa Upinzani nchini Msumbiji,Venancio Mondlane amerejea nchini humo Alhamisi kutoka uhamishoni wakati vikosi vya usalama vikifyatua mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya  wafuasi wake.

Mondlane aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais, alionekana akishuka kutoka kwenye ndege katika uwanja wa ndege wa Mavalane, ulioko kwenye mji mkuu wa Maputo.

SOMA: Wapinzani Msumbiji kuandamana kupinga uchaguzi

Kiongozi huyo wa upinzani aliondoka nchini humo mwezi Oktoba baada ya uchaguzi mkuu uliokumbwa na utata na kusababisha maandamano makubwa ya vurugu yalioitumbukiza nchi hiyo katika mzozo.

Amesema aliondoka nchini humo kwa kuhofia usalama wa maisha yake baada ya wanachama wawili waandamizi wa chama chake cha upinzani kuuawa na watu wasiojulikana mara tu baada ya uchaguzi.

Habari Zifananazo

Back to top button