VETA kuadhimisha miaka 30 elimu ya ufundi

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ametangaza kuanza kwa Maadhimisho ya miaka 30 ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na miaka 50 ya Utoaji Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Akizungumza leo Machi 05 jijini Dar es Salaam Prof. Mkenda amesema Maadhimisho hayo yanafanyika wakati Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo ya kuhakikisha vyuo vya VETA venye hadhi ya mikoa vinajengwa katika mikoa yote na vya hadhi ya wilaya vinajengwa katika wilaya zote nchini.
Prof. Mkenda amesema katika kutekeleza agizo hilo Serikali inakamilisha Chuo cha VETA katika Mkoa wa Songwe ambao haukuwa na chuo hicho na pia kuendelea na ujenzi wa vyuo vya wilaya 64 katika wilaya ambazo hazikua na vyuo vya VETA.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button