MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Kampasi ya Dar es Salaam imebuni kifaa maalumu cha kupima uwezo wa kufikiri kwa watu wenye mahitaji maalum.
Akizungumza na HabariLeo leo Julai 2, 2023 katika banda la Veta kwenye Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara, mwalimu Kintu Kilanga amesema kifaa hicho kinarahisisha kutambua uwezo wa mtoto mwenye ulemavu na kujua tatizo lipo wapi na wao kuanza kumfundisha.
“Duniani kuna njia mbili ya kujifunza ipo ya kuonesha namna mtu anavyofanya na kujifunza na pia ipo ya uwezo wa kugundua kina cha uelewa,”amesema.
Amesema sababu kubwa ya kubuni kifaa hicho ni kutokana na kuona jamii haitambui aina ya ulemavu ambao watoto wao wanao na kujua kuwa wana aina moja ya ulemavu.
Kwa upande wa mwalimu msaidizi wa wanafunzi hao ambaye amejitambulisha kwa jina moja la Paulo amesema mwanafunzi mwenye uhitaji anapofika chuoni kwao upelekwa katika kifaa hicho na kupimwa uwezo na wao kujua namna ya kuanza kumfundisha.
“Tunaamini kuwa pale mtu anapofanya kazi fulani ndo anajifunza hivyo kifaa hiki kinamfanya mtoto mwenye ulemavu kujifunza vitu vingi,”amesema.
Aidha amesema hadi sasa kasi ya uandikishaji kwa chuo chao ipo vizuri kwa kundi hilo kutokana na elimu wanayoendelea kuitoa katika maonesho hayo kila mwaka ambapo wamefikia wanafunzi 22 kwa mwaka huu.
Comments are closed.