Vifaa vya utafiti wa maji chini ya ardhi vyaongezwa

DODOMA: Serikali ya Tanzania imetolewa vifaa vya kisasa vya utafiti wa maji ya chini ya ardhi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 5 kwa Wakurugenzi wa Maji ya Mabonde kama sehemu ya jitihada za kuimarisha upatikanaji wa maji kupitia tafiti za kisayansi na teknolojia ya kisasa.

Vifaa hivi, vilivyonunuliwa kupitia  fedha za UVIKO zilizotolewa Shirika la Fedha Duniani (IMF) wa Benki ya Dunia, vilikabidhiwa rasmi leo, Mei 9, 2025, mjini Dodoma na Waziri wa Maji, Mheshimiwa Juma Aweso.

Vifaa hivi vitasambazwa katika mabonde nane ikiwemo bonde la  Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria, Wami-Ruvu, Rukwa, Ruvuma, Rufiji, na Bonde la Kati.

Seti moja itabaki makao makuu ya Wizara ya Maji mjini Dodoma ili kusaidia tafiti za kuendelea na Idara ya Rasilimali za Maji, ili kushughulikia ongezeko la mahitaji ya maji.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mheshimiwa Aweso alisema kuwasili kwa vifaa hivi uwepo wa vifaa hivi utasaidia kufanya tafiti ili kuyapata maji yaliyopo chini ya ardhi ili kuweza kuwanufaisha watanzania.

“Nchi ina takriban mita za ujazo bilioni 21 za maji ya chini ya ardhi, lakini sehemu kubwa bado haijachimbwa kutokana na ukosefu wa teknolojia bora na upungufu wa tafiti sahihi. Miji kama Liwale na Kilindi zilikuwa zikidhaniwa kuwa hazina maji, lakini utafiti wa kina umeonyesha vinginevyo,” alibainisha.

Waziri Aweso alisisitiza kuwa kwa kutumia teknolojia hii mpya, Wizara ya Maji sasa haina visingizio vya kushindwa kugundua vyanzo vya maji, na aliwahimiza wataalamu wa mabonde kuhakikisha kuwa vifaa hivi vinatumiwa kikamilifu.

“Vifaa hivi si vya kukaa tu kwenye masanduku au makabati wakisubiri wageni wakuu kuja kuona. Ninyi ni wataalamu, na nina imani na uwezo wenu. Tayari mmeonyesha mafanikio kwenye maeneo magumu. Sasa tuangalie maeneo yaliyobaki na kuhakikisha kila kijiji kinapata maji safi,” alisisitiza.

Alitaja maeneo kama Mkonze, Nala, Nzuguni, na Ilazo jijini Dodoma kuwa ni maeneo ya kipaumbele kwa ajili ya utafiti wa maji chini ya ardhi kutokana na mahitaji yanayoongezeka kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu.

Aidha, Waziri Aweso aliwahimiza Wakurugenzi wa Mabonde kuhakikisha kuwa vifaa hivyo vinatumika kwa madhumuni yake na kuonyesha dhamira ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa Watanzania wote.

“Tuweke  nguvu zetu kwa vijiji vyote 1,500 vilivyobaki. Kupitia Shirika la Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA), tumefikia zaidi ya vijiji 10,500 kati ya 12,318. Mashine na vifaa hivi vya kisasa vipo, tuvitumie kukamilisha dhamira ya kumwondoa mama kutoka na ndoo kichwani,” alisisitiza.

Waziri Aweso aliongeza kuwa, Wizara itajitahidi kuwekeza zaidi katika kujenga uwezo wa tafiti ili kuharakisha ugunduzi wa maeneo bora ya maji ya chini ya ardhi, katika maeneo ya mijini na vijijini.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Dkt. George Lugomela, alitoa pongezi kwa serikali kwa kuhakikisha wizara inapata vifaa vya kisasa vitakavyoongeza ufanisi wa tafiti za maji ya chini ya ardhi.

Hata hivyo, Dkt. Lugomela alionyesha wasiwasi kuhusu ukosefu wa vifaa na miundombinu katika ofisi za mabonde, akisema kuwa nyingi yao zina ofisi chache za wilaya, ambazo mara nyingi zipo mbali na makao makuu ya bonde na kukosa vifaa muhimu kwa ajili ya tafiti za maji ya chini ya ardhi.

“Tunaomba msaada zaidi katika kupata vifaa vya ziada ili kuboresha ufanisi wetu katika tafiti za maji ya chini ya ardhi na shughuli za kuchimba visima,” alisema.

Vifaa vilivyonunuliwa ni pamoja na magnetometer kwa ajili ya kugundua mapengo kwenye miamba, terrameter kwa ajili ya kugundua maji, kifaa cha kupima kina cha maji, kifaa cha kufuatilia mtiririko wa maji ya chini ya ardhi, na kifaa cha GPS cha kurekodi viashiria vya kijiografia.

Habari Zifananazo

One Comment

  1. I was BROKE and desperate… now I make $3,000+ weekly from my couch! Just 30 days ago, I was stuck in a dead-end job, living paycheck to paycheck. Then I found this secret method—and everything changed Anyone can do this in their free time. Spots are LIMITED! Don’t miss out!

    Join now➤➤ 𝐖­𝐰­𝐰­.­𝐄­𝐚­𝐫­𝐧­𝐀­𝐩­𝐩­𝟏­.𝐜­𝐨­𝐦

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button