KAMATI ya Uongozi ya Chama cha ACT-Wazalendo imekutana leo katika Ukumbi wa Juma Duni Haji ulioko katika Jengo la Maalim Seif Makao Makuu ya chama hicho Magomeni Dar es salaam.
Kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu ameongoza kikao hicho kilichojaa vigogo wa ACT Wazalendo ikiwa ni mikakati kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na vitongoji utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Viongozi waliohudhuria kikao hicho ni Mwenyekiti wa Taifa na Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud, Makamu Mwenyekiti Bara, Isihaka Mchinjita, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, Ismail Jussa, Katibu Mkuu, Ado Shaibu, na manaibu wake wa wawili Bara na Zanzibar.
Pia wamehudhuria viongozi wastaafu, Zitto Kabwe, na Juma Haji Duni.