Vijana wa kike washauriwa kujiwekeza

VIJANA wa kike wameshauriwa fedha wanazopata watumie kufanya uwekezaji ili kuwajengea uwezo wa kujitegemea kwa ajili ya maisha yao ya baadaye.
Ziana Mlawa, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Wizara ya Nishati ametoa ushauri huo leo Machi 2, 2025 alipozungumzia nafasi ya msichana kuelekea Maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani yatakayofanyika mkoani Arusha.
“Pamoja na majukumu yetu tuliyokuwa nayo tukijiwezesha na sisi kwenye uwekezaji itatujengea sana kujiamini kwenye kufanya kazi, ukiwa na uhuru wa kifedha kujiamini kunaongezeka kwenye kazi yako,” ameshauri mkurugenzi huyo.
Mlawa amesema Wizara ya Nishati inaitekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya ‘Wanawake na Wasichana 2025 Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji’ kwa namna mbalimbali ikiwemo suala la usawa.
Amesema wizara ina watumishi wanawake wapo 82 na wanaume 145 na kueleza kuwa kwa uwiano huo kauli mbiu hiyo imefanyiwa kazi.
Ameongeza kuwa hata kwa viongozi wa Menejimenti ya Wizara ambayo idadi yao ni 12 wanawake ni watano na wanaume ni saba.


