Vijana waandamana Kenya

KENYA; Kundi la vijana limeandamana mjini Nairobi, Kenya leo Juni 20, 2024 kuishinikiza serikali kufuta mapendekezo ya muswada wa sheria ya kodi, ambao wanadai hauna tija kwa wananchi.

Vijana hao wamedai muswada huo haukushirikisha wadau wengi wakiwemo wanasiasa, ili uweze kujadiliwa kwa maslahi ya taifa jambo ambalo haliwezi kukubalika kwa mujibu wa sheria.

“Muswada huu fedha una utata na haujapangwa wala kujadiliwa na wanasiasa na huu ni uasi, “ wamedai vijana hao.

Advertisement