Vijana watakiwa kuchangamkia fursa kilimo
DAR ES SALAAM; VIJANA watakiwa kuchangamkia fursa zilizopo katika miradi ya kilimo, ili kujitengenezea ajira ya kudumu na kuachana na kusubiri kuajiriwa.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Gerald Mweli katika kongamano la vijana wanaojihusisha na kilimo nchini, lililoandaliwa na Shirika la Mageuzi ya Kijana Tanzania (AGRA) kupitia mradi wa Building a Better Tomorrow (BBT).
“Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali tumeandaa mpango maalumu kuhakikisha vijana wanajitengenezea ajira ya kudumu kupitia kilimo, na sasa hivi International Forums zote zitahusisha vijana ambapo vijana watakuwa wakisafiri nje ya nchi, ili wakajifunze namna ya kuwekeza kwenye kilimo.
“Nitoe wito kwa vijana jiajirini kwenye kilimo, kinalipa na sasa hivi baadhi ya mashirika kutoka mataifa ya nje yanataka kuleta fund kwa ajili ya vijana wa kitanzania wanaojihusisha na kilimo,”amesema Mweli.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa AGRA, Vianey Rweyendela amesema kukua kwa uchumi wa Tanzania kunatokana na shughuli za kilimo.
“Kukua kwa uchumi nchi umetokana na kilimo kwani asilimia 65 ya Watanzania wanaishi kwa kutegemea kilimo,” amesema Rweyendele.
Amesema kuwa katika kipindi cha uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, bajeti ya kikomo imeongezeka zaidi ya mara 5 tofauti na vipindi vilivyopota na kwamba lengo la kuongeza bajeti ni kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na kwamba Agra kupitia mradi wa BBT, imelenga kusaidia vijana wakulima katika upatikanaji wa masoko ,mashamba na kuwakopesha fedha ili waweze kufanya shuguli za kilimo.
Naye Emmanuel Kisinda, Mkurugenzi wa Kikomba Avocado farm, amesema wananufaika na AGRA na wapo katika mafunzo hayo kwa lengo la kujua sera za namna gani ambazo wanaweza kuona kijana asaidiwe kwenye upatikanaji wa masoko, fedha na ardhi.
Mkame Tetere ambaye ni Mkurugenzi wa Makame Limited, amesema wao kama wakulima wana changamoto mbalimbali, ambazo wanakutano nazo ikiwemo ukosefu wa mbegu kwa walikuma wa vujiji
“Tunaamini AGRA wakiweka mfumo mzuri wa kuwakopesha wakulima mbegu moja kwa moja na ambao hataweza kuwabana wakulima,” amesema Makame.