Vijiji 12,333 kushiriki uchaguzi mitaa

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa ametangaza kuwa jumla ya vijiji 12, 333, mitaa 4,269 na vitongoji 64, 274 vitashiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024.

Mchengerwa ametoa taarifa hiyo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kuongeza kuwa kwenye orodha hiyo yamejumuishwa maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa tangazo la serikali ambayo pia yalihusisha tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha.

SOMA: Ulinzi kuimarishwa uchaguzi serikali za mitaa

“Matangazo haya yanajumuisha maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa Tangazo la serikali namba 673 na 674 ambayo yalihusisha pia Tarafa ya Ngorongoro.

Lengo la hatua hii ni kuhakilisha kuwa maeneo haya yanapata uwakilishi mzuri kiutawala pamoja na huduma za kijamii na kiuchumi zinazowiana na mahitaji ya wananchi.

SOMA: INEC haina mamlaka usimamizi uchaguzi mitaa

Mchengerwa pia amesisitiza umuhimu wa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo katika kuunda serikali ya wananchi kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kujiandikisha kwa wingi kwenye daftari la mpigakura kwa mustakabali wa maendeleo na kuendeleza juhudi za serikali katika kujitafutia maendeleo endelevu.

Habari Zifananazo

Back to top button