BRAZIL : VIONGOZI wa nchi zilizoendelea Kiuchumi Duniani (G20), wametoa wito wa kusitishwa mapigano katika Ukanda wa Gaza na nchini Lebanon.
Wito huo wa viongozi wa G20 umetolewa sambamba na kuachiliwa kwa mateka na kuruhusu raia kurejea salama katika makazi yao.
Aidha viongozi hao waliokutana mjini Rio de Janeiro nchini Brazil, wamesema katika taarifa yao ya pamoja kwamba wanahimiza mipango yote muhimu na yenye kujenga ambayo inaunga mkono amani ya kina, ya haki na ya kudumu nchini Ukraine.
Tamko hilo linaeleza kuwa amani ya aina hiyo inapaswa kuendana na kanuni za Umoja wa Mataifa na kukuza mahusiano mema, ya amani na kirafiki baina ya nchi jirani.
Hayo yanajiri wakati vita vya Gaza, Lebanon na Ukraine vikiendelea kusababisha maafa makubwa.