Viongozi upinzani Senegal wapinga uchaguzi kuahirishwa

VIONGOZI wa upinzani nchini Senegal wameungana kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais, mmoja wa wagombea, Anta Babacar, amesema.

Takriban wagombea 12 kati ya 20 wa urais walioidhinishwa kugombea katika uchaguzi mkuu wa Februari na wamekubali kuweka tofauti za kisiasa kando ili kupambana na ucheleweshaji huo, Babacar alisema, akiongeza kuwa changamoto za kisheria na maandamano makubwa huenda yakafanyika.

“Hatujadili. Hatujadili. Hatuahirishi. Ni tarehe moja na tunaishikilia,” alisema mjasiriamali huyo anayeongoza vuguvugu la kisiasa.

Advertisement

“Sasa hivi, tunajiandaa, tunapika. Kwa hiyo, mtu asidanganywe na amani hii mitaani,” Babacar alisema.