Viongozi wa dini watakiwa kuepuka uchochezi uchaguzi mkuu

DAR ES SALAAM: VIONGOZI wa dini nchini wametakiwa kuepuka kauli za uchochezi katika kipindi kuelekea uchaguzi mkuu, pamoja na kutokuingilia kazi za vyombo vya dola.

Wito huo umetolewa leo na Askofu Philipo Mafuja wa Kanisa la AICT, Dayosisi ya Pwani, katika kongamano la amani kwa viongozi wa dini, lililofanyika kujadili nafasi ya viongozi wa dini katika kudumisha amani kuelekea uchaguzi mkuu.

“Ili kuepuka kauli ambazo zinaweza kupelekea uvunjifu wa amani nchini, viongozi wa dini tunapaswa kuwa makini na kile tunachokisema kwa waumini wetu. Tumeaminiwa, hivyo ni muhimu kutumia majukwaa yetu kuhubiri amani na mshikamano,” amesema Askofu Mafuja.

Aidha, amewaonya viongozi wa dini kuacha kuingilia masuala ya kisheria, hasa katika kipindi hiki ambapo baadhi ya wanasiasa hujitokeza kwenye nyumba za ibada au kuwaalika viongozi wa dini katika majukwaa yao ya kisiasa.

“Tunapaswa kuwa waangalifu na kuzingatia kwamba akili ya kwenye siasa haiwezi kuletwa kwenye dini,” ameongeza.

Katika kongamano hilo, suala la ushiriki wa wanawake kwenye siasa pia lilijadiliwa. Mwanaharakati wa haki za wanawake, Shamim Khan, amesema kuwa mazingira ya uchaguzi bado si rafiki kwa wanawake kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo matusi na vitendo vya udhalilishaji.

“Kutokana na hali hiyo, bado kuna haja ya kuendelea na mfumo wa viti maalum kwa ajili ya wanawake. Sikutegemei hoja ya kuviondoa viti maalum kwa sasa, kwani bado havijafikia mazingira ya usawa katika nafasi za kuchaguliwa,” amesema Shamim.

Hata hivyo, amewahimiza wanawake kuendelea kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika michakato ya uchaguzi ili kuongeza ushiriki wao katika uongozi wa taifa.

Habari Zifananazo

2 Comments

  1. Hey there just wanted to give you a brief heads up and let you know a few of the images aren’t loading properly.
    I’m not sure why but I think its a linking issue. I’ve tried it in two different internet browsers and both show the same results.

  2. Hi, I doo think this iss an excellent site. I stumbledupon it 😉 I
    aam goig to coe back yett gain sjnce Ibook-marked it. Money and freedolm
    is the best way tto change, mmay you bee rich and continue
    tto guide other people.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button