NAIBU Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel, amewaomba viongozi wa dini nchini kushirikiana na serikali kutoa elimu ya lishe bora kwa waumini wao, kwa lengo la kuhamasisha matumizi bora ya chakula, ili kuwa na afya bora.
Dk Mollel alisema hayo mwishoni mwa wiki, katika hotuba yake kwenye maadhimisho ya siku ya lishe kitaifa, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kijiji cha Fulwe, Tarafa ya Mikese , Wilaya ya Morogoro.
Naibu Waziri hiyo alimwakilisha Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu na kauli mbiu ya mwaka huu ilibeba ujumbe wa Lishe Bora Ni Msingi wa Maendeleo Eendelevu: Sote Tuwajibike.
“ Nitumie fursa hii kuwaomba watumishi wa Mungu kuongelea suala la lishe wakati wa ibada zenu, kuna uhusiano mkubwa wa akili na kutenda dhambi,” alisema Dk Mollel.