Viongozi wahimiza uwekezaji nishati jadidifu Afrika

MAREKANI – KATIKA mkutano wa kilele wa kimataifa wa Nishati Jadidifu (Global Renewables Summit) uliofanyika nchini Marekani, viongozi wa dunia wamehimiza mataifa mbalimbali, hasa yale ya Bara la Afrika, kuwekeza zaidi katika nishati jadidifu ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Rais wa Kenya, William Ruto, alisisitiza umuhimu wa uwekezaji katika nishati rafiki barani Afrika, akirejelea ahadi iliyotolewa kwenye mkutano wa COP28 mwaka jana ya kuongeza uwezo wa nishati safi mara tatu ifikapo mwaka 2030.

Ruto alionyesha wasiwasi kwamba Afrika inapata chini ya 50% ya uwekezaji wa kimataifa wa nishati jadidifu, licha ya kuwa na asilimia 60 ya fursa bora zaidi za nishati ya jua duniani.

Advertisement

Alisema, “Afrika ina utajiri mkubwa wa rasilimali zinazohitajika kwa maendeleo, lakini mara nyingi haiwezi kufikia rasilimali hizo kutokana na mchanganyiko wa sasa wa nishati isiyoweza kutegemewa au ya gharama kubwa.” Alisema Rais Ruto

Kiongozi huyo alisisitiza kuwa ili kufikia malengo ya nishati safi, ni muhimu kuwe na mkakati wa pamoja wa uwekezaji na ushirikiano wa kimataifa.

Hatahivyo,Rais  Ruto  amesema viongozi wa dunia wanatakiwa kuchukua hatua za dhati ili kuimarisha uwekezaji katika sekta ya nishati jadidifu ambayo itasaidia kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii barani Afrika.