Viongozi wapongeza kusitishwa kwa mapigano Gaza

QATAR : VIONGOZI mbalimbali wa dunia wapongeza makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza na kuachiliwa kwa mateka ambayo yataanza kutekelezwa rasmi Jumapili mchana.

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi, ametoa wito wa kuwasilishwa kwa msaada wa haraka wa kibinadamu katika Ukanda wa Gaza, akipongeza mpango uliofikiwa wa usitishwaji mapigano huko Gaza umetokana na juhudi za Misri, Qatar na Marekani.

Hatahivyo viongozi mbalimbali duniani wamehimiza kuchukuliwa kwa hatua za ziada baada ya kufikiwa kwa makubaliano hayo wakisisitiza kuwepo kwa juhudi za kimataifa za kuyajenga upya maeneo yaliyoharibiwa na vita.

Advertisement

Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa Mamlaka ya Wapalestina, Mohammed Mustafa, amesema Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kuendelea kuishinikiza Israel kukubali kuundwa kwa dola huru la Wapalestina.

Makubaliano hayo ya kihistoria ya kusitisha mapigano kwa muda wa wiki sita huko Gaza yanajumuisha hatua tatu ili kufanikisha kuvimaliza kabisa vita hivyo.

SOMA: Hamas yakubali rasimu ya kusitisha mapigano Gaza

Katika hatua ya kwanza kuwachiliwa kwa mateka 33 wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas pamoja na wafungwa kadhaa wa Kipalestina.

Viongozi mbalimbali wa dunia wamepongeza makubaliano hayo wakisema yanatoa matumaini kwa raia wa pande zote ambao wamepitia mateso makubwa na kwamba yatasaidia kuendeleza juhudi za kufanikisha amani ya kudumu kati ya Israel na Palestina.