Hamas yakubali rasimu ya kusitisha mapigano Gaza

QATAR : KUNDI la Hamas limekubali rasimu ya makubaliano ya kusitisha vita katika ukanda wa Gaza na kuachiliwa huru kwa mateka.

Hayo yameelezwa na maafisa wawili wanaohusika katika mazungumzo hayo yanayofanyika mjini Doha, Qatar.

Wapatanishi wa Marekani na mataifa ya Kiarabu wamesema Israel na kundi la wanamgambo wa kipalestina la Hamas wako karibu kufikia makubaliano  hatua ambayo itaashiria kuvimalzia vita  vilivyodumu zaidi ya miezi 15.

Advertisement

Shirika la Habari la Associated Press limepata nakala ya makubaliano yaliyopendekezwa ya kusitisha mapigano, huku maafisa wa Misri na Hamas wakithibitisha uhalali wa nakala hiyo.

Afisa wa Israel amefahamisha kuwa maendeleo makubwa kuelekea kufikia makubaliano hayo yamepatikana, japo maelezo ya mwisho bado yanafanyiwa kazi. SOMA: Israel haijajibu kusudio la Hamas kusitisha mapigano

Maafisa hao wote watatu wa Misri, Hamas na Israel, wamezungumza kwa sharti la kutotajwa majina.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony  Blinken anaamini kuwa wanakaribia kufikia makubaliano ya kusitisha mapigano na kuongeza kwamba, uamuzi huo uko mikononi mwa Hamas.

Amesema, “Tuko karibu sana. Karibu zaidi kuliko wakati wowote ule, taarifa rasmi inaweza kutolewa aidha ndani ya saa chache au masiku.”