ISRAEL haijasema chochote kuhusiana na mpango wa kundi la wanajeshi wa Palestina Hamas juu ya kusitisha mapigano kwa siku nne kuanzia kesho Alhamisi.
–
Hamas wameeleza nia ya kusitisha mapigano hayo huku ikingoja kauli ya Israel kuhusu makubaliano.
–
Wakati Hamas wakiwa na kusudio hilo, Israel inataka kuachiwa kwa mateka wao wa kwanza na wanatarajia kuwapokea Alhamisi, Waziri ya Nje wa Israel, Eli Cohen ameeleza.
–
Chini ya makubaliano hayo, mateka 50 wa Israel waliotekwa na Hamas wataachiwa, wanawake na vijana 150 wa Kipalestina waliokuwa kwenye jela za Israel wataachiwa pia.
–
Familia za wale wanaoshikiliwa huko Gaza zimesema kila mateka “anahitaji kurudi nyumbani” na kwamba kila saa ni “muhimu”.
–
Israel imeendeleza operesheni yake ya ardhini na anga huko Gaza na msemaji wake mkuu wa jeshi amesisitiza kuwa vita vinaendelea.
–
Israel ilianza kushambulia Gaza baada ya wapiganaji wa Hamas kuvuka mpaka Oktoba 7 na kuua watu 1,200 na kuwachukua mateka wengine 240.
Home Israel haijajibu kusudio la Hamas kusitisha mapigano
Comments are closed.