Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amewaomba viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa kutimiza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozi inayoongoza nafasi husika ili kuleta maendeleo kwa wananchi kwa ustawi wa taifa.
Mchengerwa ametoa wito huo wakati akijibu hoja na ushauri wa wabunge alipokuwa akichangia mjadala wa mapendekezo ya mpango wa maendeleo ya Taifa na mapendekezo ya muongozo wa maandalizi ya mpango wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2025/26.
SOMA: Mchengerwa atoa maagizo kwa Wakurugenzi Halmashauri
“Ni vyema tukaheshimiana na huo ndiyo msingi wa taifa hili, uliowekwa na baba wa taifa, hivyo nisistize tuheshimiane katika nyakati zote za utendaji wetu wa kazi hasa tunapo wahudumia watanzania kama inavyosisitizwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu” amesema Waziri Mchengerwa.