Vita ya kuumbuana Chadema yashika kasi

DAR ES SALAAM; WAGOMBEA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wanazidi kuumbuana kutokana na kufichua mambo mbalimbali yanayoendelea ndani mwao.
Hayo yanatokea kuelekea uchaguzi wa nafasi mbalimbali za uon gozi hususani uenyekiti na makamu wake unaotarajiwa kufanyika Januari 21, mwaka huu.
Katika mahojiano ya Clouds 360 na mgombea wa nafasi ya Mwe nyekiti, Tundu Lissu yaliyofanyika nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam jana, alisema, Peter Msigwa alifukuzwa Chadema na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na kwamba wapo viongozi wengi walioondoka kwa sababu ya zengwe la viongozi.
Lissu amedai wanachama waliokuwa wanapinga masuala mbalimbali yanayoendelea ndani ya chama, waliandaliwa zengwe na kufukuzwa.
Amedai kuwa mgombea wa na fasi ya Makamu Mwenyekiti, Ezekia Wenje alitangaza kumuunga mkono, Mbowe kwa kuogopa kufukuzwa ndani ya chama. Lissu alisema awali hakuwa na nia ya kugombea uenyekiti, lakini kutokana na mabadiliko mbalimbali waliyoyabaini ndani ya uongozi, wanachama walimshauri kugombea.
Alisisitiza kuwa harakati za ku gombea nafasi hiyo zilianza baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na alipotangaza nia ya kugombea nafasi hiyo aliitishiwa vikao ili asitangaze nia yake.
“Nikiwa mwenyekiti nitafungua milango kwa wengi walionewa na kuondoka kwa sababu mbalimbali, na wanaosita kuwa wanachama wataruhusiwa kujiunga na chama hicho tena,” alisema Lissu.
Lissu alisema wanahitaji watu wa maana kwenye chama ambao watakiwezesha kusonga mbele katika kuchechemua mabadiliko na maendeleo wanayoyataka Hata hivyo, alisema haridhishwi na vitendo vya rushwa vinavyo fanyika katika chaguzi hizo.
“Mimi nilizungumzia rushwa watu wakapiga kelele, tumeona juzi kwenye uchaguzi wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) na nimepata taarifa kwenye ucha guzi wa wazee kuna rushwa, kura zinanunuliwa, rushwa inatembezwa watu wanakaa chooni wanagawa pesa, mambo ambayo siku zote tunayalalamikia kwenye chaguzi tunaona kwenye chaguzi za chama chetu na hiyo haiwezi kuwa jambo jema hata kidogo,” alisisitiza.
Alisema msimamo wake katika chama unajulikana na kutokana na kuzungumza ukweli, anaonekana ni tatizo kati ya watu wengi.
Naye mgombea wa Umakamu Mwenyekiti, Wenje alisema Lissu na Godbless Lema walianzisha Kampeni ya ‘Join the chain’ kwa lengo la kumpindua, Mbowe wakati alipokuwa gerezani akikabiliwa na kesi ya ugaidi
“Hiki chama kina intelligence (intelijensia), na intelligence report (ripoti ya intelijensia) ya chama chetu iliwasilisha hilo, mwenyekiti wetu ni mvumilivu na sio dhaifu, kwa sababu tunahitaji watu kuwa pamoja, kwa hiyo mtu kama, Freeman (Mbowe) na moyo wake anaweza kuvumilia,” alisema Wenje.
Alidai katika kamati hiyo ambayo mwenyekiti wake alikuwa, Lema ambaye alikusanya fedha na hazijulikani zilipo, na kwamba lengo Lissu awe mwenyekiti wa chama na Msigwa awe makamu mwenyekiti.
“Niliposhirikishwa katika suala hili nilikataa kuwa muasi, nikajion doa na ndio mwanzo wa ugomvi kati yangu na hawa marafiki zangu ambao wanasema niligeuka nyuzi 360, nilikataa kufanya mapinduzi,’’ alidai Wenje.
Alisema kama sio uvumilivu watu wanaofanya uasi kwenye vyama ndio wanaopaswa kuon dolewa, na miongoni mwao ni Lema kwa kupanga mapinduzi kinyume na katiba.
Pia, alidai Dk Wilbroad Slaa hafai kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho kwa sababu katika kitabu chake, aliandika kuwa Chadema ni chama cha utekaji, jambo ambalo ni la upo toshaji na lingechangia kufutwa kwa chama hicho.
Naye Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Katavi, Rhoda Kunchela alisema kauli iliyotolewa na mtoto wa Mbowe, James dhidi ya Lema zinaashiria ukabila akidai asipoomba radhi hadharani, italeta mapokeo tofauti ndani ya chama hicho. Itakumbukwa kuwa baada ya Lema kutangaza kuwaunga mkono Lissu na Heche, James Mbowe ali tumia ukurasa wake wa X kuandika hivi, “Nimetafakari kwa kina tabia aliyoonesha ndugu Lema jana siyo tabia za Wachaga”.
Kwa kauli hiyo, Kunchela alisema inaashiria ukabila, na ni ya kup ingwa na kila anayependa ustawi wa demokrasia na asiyekubaliana na vitendo vya ukabila.

