Vodacom yajikita uchumi wa kidijiti

DAR ES SALAAM: Kampuni ya Teknolojia na Mawasiliano Vodacom Tanzania imeendelea kujikita katikati kukuza uchumi kupitia maendeleo ya kidijiti kwa kutumia teknolojia bunifu kuongeza ujumuishwaji kifedha kwa Watanzania.
Kampuni hiyo imedhihirisha hayo leo Aprili 2,2026 kupitia uwekezaji wa mabadiliko ya mifumo katika huduma zao za kifedha kwa njia ya simu yaani M-Pesa kwa kutoka katika matumizi ya teknolijia ya awali ya G2 na kwenda Fintech 2.0.
Akizungumzia uwekezaji huo Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Philip Besiimire amesema unalenga kuijengea huduma hiyo misingi imara kwa ajili ya siku zijazo.
“Tunaimarisha huduma ya M-Pesa ili iendelee kuwa salama, ya kuaminika na yenye uwezo wa kusaidia maendeleo ya kiteknolojia. Wateja wetu wanastahili huduma inayo kua sambamba na mahitaji yao ya kasi zaidi, nguvu zaidi na uthabiti wa hali ya juu,” amesema Besiimire.
Imeelezwa kuwa mabadiliko hayo ya kiteknolojia katika huduma zao za kifedha yanaleta ufanisi zaidi na kupunguza changamoto za kukatika kwa huduma hususani pale wanapohitaji kufanya marekebisho.
Pia unakwenda sambamba na uimarishaji wa viwango vipya vya usalama ili kulinda kulinda taarifa na miamala ya wateja, na kuongeza imani katika huduma za fedha kwa njia ya simu.
Amesema kwa mawakala, wafanyabiashara na washirika wa kibiashara, maboresho haya yataleta uwezo mkubwa zaidi wakushughulikia miamala, upatikanaji wa taarifa za kina pamoja na usimamizi wa huduma ulio wazi zaidi na kusaidia kupanga biashara vizuri na kurahisisha huduma kwa wateja.




JOIN US Everybody can earn 250/h Dollar + daily 1K… You can earn from 12000-16700 Dollar a month or even more if you work as a part time job…It’s easy, just follow instructions on this page, read it carefully from start to finish… It’s a flexible job but a good earning opportunity. tab for more detail thank you……..
.
This is my main concern…………………… http://Www.Cash54.Com
I just came across this amazing way to earn $11,000-$15,000 a month online! No selling, no struggle—just a simple system that anyone can follow. Mia Westbrook did it, and so can you! Don’t miss out on this life-changing opportunity.
.
This is what I do…………………… http://Www.Payathome9.Com