Vyama vya ushirika vyatakiwa kutumia mfumo kidigitali

VYAMA vya Ushirika vimeagizwa kutumia Mfumo wa Kidigitali wa  Usimamizi wa Vyama vya Ushirika ( MUVU) ili kuwezesha upatikanaji wa maendeleo na ukuaji wa uchumi kupitia Tehama ikiwemo ongezeko la wanachama.

Agizo hilo limetolewa leo na Kaimu Naibu Mrajis  wa Vyama vya Ushirika Uhamasihaji, Consolata Kiluma wakati wa ufunguzi wa kikao cha sita cha watendaji wakuu na mameneja wa vyama vya Uushirika wa akiba na mikopo nchini kinachofanyika kwa siku tatu Arusha.

Amesema endapo mifumo hiyo ya kidigitali ikitumiwa ipasavyo itawezesha vyama hivyo kukua na kusaidia wanachama kujikwamua kuuchumi ikiwemo taarifa za vyama kutosamba nje ya mfumo husika

Amesema awali kupitia mfumo wa MUVU idadi ya wanachama inasomeka milioni 2.3 ilhali katika uhalisia wanachama wa vyama vya ushirika wapo jumla ya milioni 8 hivyo ni vema wanachama hao wakaingizwa katika mfumo ikiwemo kufunga vizuri hesabu za vyama kwamujibu wa maelekezo yaliyotolewa na mrajis wa vyama vya ushirika.

Naye Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Akiba na Mikopo (SCCULT), Ernest Nyambo ametoa maagizo saba ya kimkakati ikiwemo ongezeko la wanachama, matumizi sahihi ya Tehama, ukuaji wa fedha na uendelevu,

Ikiwemo kuchochea utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu kwenye ujumuishi na mazingira, udhibiti wa viatarishi na ufuataji wa sheria, ukuaji wa taasisi na utawala bora pamoja na soko na mahusiano kwa umma kwani ushirika ni biashara.

Habari Zifananazo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Back to top button